Ad Code

TANGAZA NA KANKONO MEDIA HAPA 0659671919

KATIBU MKUU UVCCM CDE.JOKATE ALAMBA UTEUZI



KATIBU MKUU UVCCM CDE.JOKATE ALAMBA UTEUZI 


kankonomediabogspot.com Novemba 12.2024 - DODOMA


Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Cde. Jokate Mwegelo amechaguliwa kuwa Mratibu wa Vijana katika Shirika la Kimataifa la Women's Academy for Africa (WAFA) ambapo pia atakuwa Mjumbe wa kamati tendaji ya WAFA.




Cde. Jokate amepata nafasi hiyo katika mkutano wa kimataifa wa WAFA uliofanyika Novemba 06, 2024 nchini Botswana ambapo aliteuliwa kushiriki na Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Idara ya NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.




Cde. Jokate ameishukuru CCM kwa kuendelea kuwa na imani na vijana na hata kumteua kuwakilisha katika mkutano huo kwani imefungua fursa ya kuwavuta vijana katika Mashirika ya Kimataifa yenye Urafiki mwema na CCM na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.



Akitoa hotuba yake Jokate aliangazia mambo matano ya malengo, mkakati na maono ya WAFA kwa vijana wa kike Afrika na wanawake kwenye masuala ya siasa na uchumi.


Mosi alitaka kuendelea kufanya tathmini za kina za mahitaji katika kila nchi iliyolengwa na kubuni moduli zinazofaa, pili kuweka vigezo vya uwazi na viwango vya uteuzi wa washiriki, kwa kutambua utaalamu wa vyama vya siasa katika kuwabaini wagombea wanaotarajiwa, tatu  kustawisha mkabala wa kimaadili zaidi unaolenga muktadha mbalimbali kwa kufanya uchambuzi wa uchumi wa kisiasa ili kuelewa changamoto na fursa mahususi zinazowakabili wanawake.


Cde. Jokate alitaja jambo la nne ni kugundua usaidizi zaidi wa kifedha wa moja kwa moja kwa wagombea wa kike katika nchi zilizo na mafanikio ya kutosha katika uchaguzi na mwisho ni kutengwa fedha maalum kwa ajili ya shughuli za ufuatiliaji na tathmini ndani ya bajeti ya WAFA.


WAFA ni Mtandao unaojitolea kuendeleza Usawa wa Kijinsia kupitia uwezeshaji wa Kisiasa wa Wanawake wanaohusishwa na Vyama vya Siasa kupitia programu maalum za mafunzo kwani inalenga zaidi kuongezea Wanawake Ujuzi katika maeneo yanayohusiana na Demokrasia, Uongozi, kukuza na kuongeza Ushiriki wa Wanawake katika Vyama vya Siasa na Kugombea nafasi mbalimbali za Uongozi likifanya kazi zake kwa kushirikiana na Westiminster Foundation for Democracy (WFD) na UK Labour Party.



#KankonoMediaNewsUPDATES


Post a Comment

0 Comments