![]() |
RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MWINGINE
kankonomediablogspot.com mei.08.2025 - DAR ES SALAAM
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Africa Media Group, Shaaban Kissu kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Taarifa ya uteuzi wa Kissu, imetolewa leo Mei 7, 2025 Ikulu, Dar es Salaam na Katibu wa Rais, Waziri Salum katika hafla ya chakula cha mchana kati ya Rais Samia na waandishi wa habari walioshiriki tuzo za Samia Kalamu Awards.
Katika taarifa hiyo, Salum amemtambulisha Kissu katika wadhifa huo mpya, huku akisema uteuzi wake umefanywa leo na hata mwenyewe hakuwa na taarifa.
"Hii taarifa nafikiri ni surprise hata kwa Kissu mwenyewe, kwa sababu hakuwa na taarifa. Hata mmeona nimechelewa kufika hapa tulikuwa tunashughulikia mambo hayo," amesema Salum
#KankonoMediaNewsUPDATES#KankonoTvNewsUPDATES
0 Comments