Ad Code

TANGAZA NA KANKONO MEDIA HAPA 0659671919

KAWAIDA: CCM CHAMA CHENYE USHAWISHI KWA VIJANA TANZANIA



KAWAIDA: CCM CHAMA CHENYE USHAWISHI KWA VIJANA TANZANIA



kankonomediablogspot.com Mei.19.2025 - MJINI MAGHARIBI - ZANZIBAR 



Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Ndg. Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) kimeendelea kuwa na mvuto na ushawishi kwa rika mbalimbali hususani vijana wa Tanzania kutokana na utekelezaji mkubwa wa ilani ya mwaka 2020-2025.


Ndg. Kawaida amesema hayo jana tarehe 17 Mei 2025 mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati akizindua tawi jipya la CCM la Mpendae mkoa wa Mjini Magharibi.


Ndg. Kawaida amesema utekelezaji wa ilani unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi umeongeza mvuto, ushawishi kwa vijana na kuvuna wanachama wengia kushinda chama chochote cha siasa.


Amewahakikishia viongozi hao kuwa ikifika Oktoba 2025 wajiandae kupata ushindi wa kishindo kutoka kwa kundi kubwa la vijana wa Tanzania.


#KankonoMediaNewsUPDATES#KankonoTvNewsUPDATES

Post a Comment

0 Comments