Ad Code

TANGAZA NA KANKONO MEDIA HAPA 0659671919

RAIS SAMIA ASAMEHE FAINI ZA MAJI NCHI NZIMA




RAIS SAMIA ASAMEHE FAINI ZA MAJI NCHI NZIMA 


kankonomediablogspot.com mei.08.2025 - DODOMA 


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesamehe faini za maji kwa Wananchi wote wenye faini katika Mamlaka za Maji nchini hivyo wenye faini wameombwa kufika kwenye Mamlaka hizo kwa ajili ya kurejeshewa huduma ya maji ambapo wanatakiwa kufika kuanzia sasa hadi May 31,2025.




#KankonoMediaNewsUPDATES#KankonoTvNewsUPDATES


Waziri wa Majl, Jumaa Aweso ametangaza msamaha nuo kutoka kwa Rais, leo May 08,2025 wakati akiwasilisha Bungeni Jijini Dodoma Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Maji kwa Mwaka 2025/2026.


Aweso amesema "Ninapenda kutoa salaam za Wizara ya Maji kwa Wananchi wote wenye faini katika Mamlaka za Maji kuwa Mama Samia amesamehe faini hizo na hivyo wafike kwenye Mamlaka kwa ajili ya utaratibu wa kurejeshwa huduma ya maji hadi tarehe 31 Mei 2025"


"Wateja wote wenye madeni kwenye Mamlaka za Maji (ikiwemo waliokatiwa maji kisa madeni) wafike ofisini kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kulipa madeni yao na kurejeshwa huduma mara moja

Post a Comment

0 Comments