Ad Code

TANGAZA NA KANKONO MEDIA HAPA 0659671919

KIGOGO MWINGINE WA CHADEMA ATIMKIA CCM




KIGOGO MWINGINE WA CHADEMA ATIMKIA CCM 


kankonomediablogspot.com April 27.2025 - TARIME - MARA



Kiongozi mwandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kutokea Tarime, mkoani Mara, Mohania Joseph Peter, amekianga chama hicho, akisema ni cha kiharakati na hakiwezi kufanya siasa.



Ndugu Mohania, ambaye amewahi kushika nafasi mbalimbali katika chama hicho ngazi ya mkoa, katika Baraza la Vijana wa Chama hicho (Bavicha), kabla ya kuwa msaidizi katika ofisi ya chama hicho Mkoa wa Mara, amesema chama kinachoendekeza harakati kinajiandaa kufa kisiasa na hakiwezi kuaminiwa kushika dola.



Kiongozi huyo amesema hayo, alipopewa nafasi ya kuzungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, katika Uwanja wa Shamba la Bibi, mjini Tarime, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, ambapo pia alitangaza uamuzi wa kuhama Chadema, akijiunga na CCM.


“Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Mara. Nimekuwa Mwenyekiti wa Bavicha Jimbo la Tarime"-Mohania Peter 



#KankonoMediaNewsUPDATES#KankonoTvNewsUPDATES

Post a Comment

0 Comments