𝗪𝗔𝗧𝗢𝗧𝗢 𝗪𝗔 𝗞𝗜𝗞𝗘 𝗪𝗔𝗡𝗨𝗙𝗔𝗜𝗞𝗔 𝗡𝗔 𝗨𝗪𝗘𝗣𝗢 𝗪𝗔 𝗦𝗛𝗨𝗟𝗘 𝗭𝗔 𝗦𝗘𝗞𝗢𝗡𝗗𝗔𝗥𝗜 26 𝗭𝗔 𝗥𝗔𝗜𝗦 𝗗𝗞𝗧. 𝗦𝗔𝗠𝗜𝗔
kankonomediablogspot.com Julai 12.2025 - DODOMA
𝙏𝙨𝙝 𝙏𝙧𝙞𝙡𝙞𝙤𝙣𝙞 1.2 𝙯𝙞𝙢𝙚𝙩𝙚𝙣𝙜𝙬𝙖 𝙠𝙬𝙖 𝙪𝙟𝙚𝙣𝙯𝙞 𝙬𝙖 𝙨𝙝𝙪𝙡𝙚 1,026 𝙯𝙖 𝙎𝙚𝙠𝙤𝙣𝙙𝙖𝙧𝙞
Serikali ya Awamu ya sita ya Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. 𝗗𝗸𝘁. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻, imetumia shilingi bilioni 106.6 katika ujenzi wa shule 26 za sekondari za wasichana zenye mabweni, moja katika kila mkoa.
Mpango huu ni sehemu ya jitihada za serikali kuboresha elimu kwa wasichana na kuongeza fursa za masomo kwao. Kwa mfano, mkoani Ruvuma, serikali imetumia shilingi bilioni 4.35 kujenga shule ya mfano ya wasichana.
Kwa ujumla, serikali imetenga jumla ya shilingi trilioni 1.2 kwa ajili ya kujenga shule mpya za sekondari 1,026, ambapo kati ya hizo, shule 26 zimetengwa mahususi kwa ajili ya wasichana zenye mabweni katika kila mkoa.
Hadi sasa, shule 25 kati ya 26 zimekamilika na wanafunzi wameripoti shuleni, ikionyesha maendeleo makubwa katika utekelezaji wa mpango huu.
Hii inaonyesha jitihada za serikali katika kuboresha elimu ya wasichana nchini.
#KankonoMedia#KankonoTvNewsUPDATES


0 Comments