Ad Code

TANGAZA NA KANKONO MEDIA HAPA 0659671919

REHEMA SOMBI AMPONGEZA DR.SAMIA KWA KUULINDA UMOJA WA KITAIFA NA KUITUNZA AMANI YA NCHI.




REHEMA SOMBI AMPONGEZA DR.SAMIA KWA KUULINDA UMOJA WA KITAIFA NA KUITUNZA AMANI YA NCHI.


Makamu mwenyekiti wa UVCCM TAIFA Comrade REHEMA OMARY SOMBI siku ya jana Oktober 20- 2024 alikuwa mgeni rasmi wa mjadala wa kitaifa uliofanyika kupitia Group la WHAT SAPP Maarufu Kwa jina la "Friend's of Angelo Madundo" uliohusu Mada ya "HISTORIA YA BABA WA TAIFA HAYATI MWALIMU JULIAS KAMBARAGE NYERERE"



 Ambapo pia wadadisi wa mjadala walikuwa ni Mwl. DOKTA WILGIS NDUNGURU, Mhadhiri mwandamizi wa Chuo kikuu Cha kumbukumbu  ya Mwalimu Nyerere Kigamboni-DSM, Mwl. ABEL MAGEMBE LUGIMBA, Mwahistoria na Mchambuzi wa siasa za kimataifa kutoka Chuo Kikuu Cha (NORTHEAST UNIVERSITY) nchini CHINA, Mwl. EMANUEL MGASE, Mkuu wa chuo Cha Maendeleo ya Jamii na mifugo-(Mafinga-Iringa), pia Mwanahistoria, mtafiti wa Maendeleo ya Jamii, Mwl. PATRICK MASANJA, Mhe. Diwani wa Kata ya mitundu- SINGIDA, Mchambuzi wa sera na sayansi ya Jamii Pamoja na kusimamiwa na Mwenyekiti Mjadala Mwl. SHABAN LISU- kutoka Mkoa wa DSM.



Akitoa neno la ufunguzi wa mjadala huo, comred  REHEMA SOMBI, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DAKTARI SAMIA SULUHU HASSAN Kwa kazi kubwa na nzuri ya kusimamia Mageuzi na Maendeleo ya watanzania pamoja na kusimamia vyema Suala la ulinzi, usalama na amani ya taifa letu, huku akiwaomba watanzania wote kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita, katika juhudi mbalimbali za kukuza uchumi wa nchi, huduma za jamii, Demokrasia na utawala Bora,


Makamu mwenyekiti SOMBI, amewataka vijana wa kitanzania Kuishi katika jukwaa la uzalendo kama ilivyo kuwa Kwa baba wa taifa Hayati Mwalimu JULIA'S KAMBARAGE NYERERE ambae alitumia muda Mwingi kuwajenga watanzania katika Hali ya umoja na mshikamano, Uzalendo, Uchapakazi, na kupinga mgawanyiko wa matabaka ya Jamii ikiwemo, udini, ukabila, Ueneo, ukanda na urangi.



#KankonoMediaNewsUPDATES

Post a Comment

0 Comments